China kurejesha amani kwa Wapalestina kupitia UN
6 Novemba 2023China imesema itafanya kadri ya uwezo wake kurudisha amani katika maeneo ya Wapalestina wakati ikitwaa uwenyekiti wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.
Hayo yameelezwa na wizara yake ya mambo ya nje leo Jumatatu katika wakati ambapo mivutano imeongezeka katika eneo la mashariki ya Kati.
Soma pia:China na Urusi waikosoa Marekani katika mkutano wa kijeshi
Msemaji wa wizara hiyo Wang Wenbing amewaambia waandishi habari kwamba China itafanya kila iwezalo katika uwezo wake kuwashawishi wanachama wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kutimiza wajibu wao, kufanya majukumu yao na kujenga maridhiano,pamoja na kuchukua hatua zinazistahiki, haraka iwezekanavyo kutuliza mgogoro wa hivi sasa na kulinda usalama wa raia,ili kurudisha amani.
Taarifa ya China imekuja wakati Israel ikizidisha opreösheni yake ya kijesho dhidi ya kundi la Hamas.
China ilitwaa uwenyekiti wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wiki iliyopita,nafasi ambayo ni ya kupokezana.