China, Japan zadhamiria kuimarisha uhusiano
11 Oktoba 2024Japan na China zimekuwa zikijaribu mataifa hayo mawili yakijaribu kulainisha misimamo yao mikali kwenye uhasama wao wa muda mrefu.
Akizungumza na mwenzake wa Japan, Shigeru Ishiba, kandoni mwa mkutano wa Jumuiya ya Mataifa ya Kusini na Mashariki mwa Asia (ASEAN) mjini Vientiane nchini Laos, Li alisema matarajio yake ni kuwa nchi hizo mbili zinaweza kuendelea kujadiliana na kushirikiana kwa maslahi ya utulivu, maendeleo ya viwanda na mfumo huru wa biashara.
Soma zaidi: Japan yalalamikia 'harakati za jeshi' China
Kwa upande wake, Ishiba alisema Japan iko tayari kushirikiana na China na kutatuwa vikwazo vilivyopo kwenye ngazi za zote.
Mazungumzo ya mawaziri hao wakuu yamefanyika siku moja tu baada ya hapo jana mawaziri wao wa mambo ya kigeni kupigiana simu.