1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China imeleta bidhaa, barabara, sasa Afrika yataka ajira

Admin.WagnerD22 Julai 2013

Licha ya China kuleta bidhaa za bei nafuu, barabara na hata shule barani Afrika, serikali za bara hilo zinaishinikiza nchi hiyo itoe kile Waafrika wengi wanachokihitaji: Ajira.

https://p.dw.com/p/19Bul
Chinese woman stand in front of a billboard which promotes the upcoming China-Africa summit meeting, outside a hotel in Beijing Thursday Oct. 26, 2006. Beijing is making unusually lavish efforts to welcome leaders and officials from 48 African nations this week for a landmark summit meant to highlight China's huge and growing role in Africa. The Chinese characters at left read "Africa." (AP Photo/Greg Baker)
China Afrika Wirtschaft Plakat in Peking für wirtschaftliche ZusammenarbeitPicha: AP

Ripoti ya hivi karibuni iliyotolewa na tume ya uchumi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Afrika UNECA, ilibainisha hatari kuwa uhusiano wa bara hilo na taifa la China lenye uchumi wa pili kwa ukubwa duniani, unaweza kukwaza juhudi la bara hilo kukuza sekta ya viwanda. Biashara kati ya China na Afrika iliongezeka kutoka dola bilioni 10 mwaka 2000, hadi kufikia takribani dola bilioni 200 mwaka huu - miaka minne baada ya nchi hiyo kuipiku Marekani kama mshirika nambari moja wa kibiashara wa bara la Afrika.

Rais wa zamani wa China Hu Jintao alipokutana na viongozi wa Afrika.
Rais wa zamani wa China Hu Jintao alipokutana na viongozi wa Afrika.Picha: AP

Lakini asilimia 85 ya mauzo ya Afrika kwenda nchini China ni malighafi kama vile mafuta na madini. Kwa mujibu wa benki ya dunia, asilimia kubwa ya madini yanayochimbwa barani Afrika yanasafirishwa yakiwa ghafi, hii ikimaanissha kuwa ajira na utajiri vinavyotokana na kuyasafisha vinatengezwa sehemu nyingine. Wakati huo huo mtiririko wa bidhaa za China umechochea kushuka kwa uendelezaji wa sekta ya viwanda tangu miaka ya 1980.

Afrika Kusini nayo yalia na China

Hata katika taifa lenye nguvu kubwa zaidi kiuchumi barani humu, Afrika Kusini, karibu asilimia 40 ya viatu na mavaazi vinatokea China. Akielezea wasiwasi wa serikali nyingi za Afrika, rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma alionya mwaka uliyopita, kwamba mwelekeo huu wa biashara usio na urari siyo endelevu.

Ni kweli kwamba ukuaji wa China umeleta manufaa kwa bara la Afrika. Utawala mjini Beijing umesifiwa na serikali nyingi kwa utayari wake wa kufadhili miradi mikubwa ya miundombinu pasipo kuweka masharti yanayohusiana na demokrasia, utawala bora na haki za binaadamu, ambayo Afrika imekuwa ikiyakosoa katika misaada ya nchi za magharibi. Lakini fedha zake nazo zinakuja na masharti. Laazima zitumiwe kununua bidhaa za China, au kwa miundombinu inayojengwa na Wachina.

Bidhaa za bei nafuu kutoka China zinarahishisha maisha ya kila siku na kusaidia kuimarisha ununuzi barani kote. Lakini katika mataifa mengi, mahitaji ya China ya mawe yenye madini, mbao na mafuta, yamezidi kuzsukuma nchi za Afrika chini ya mnyororo wa thamani katika maeneo yaliyo na faida ndogo inayotokana na uzalishaji, na sasa NECA inasema kuna hatari ya kuzifanya chumi za Afrika kutokuwa shindani.

Juhudi zan udhibiti zagonga mwamba

Nchini Senegal, viwanda vya ndani vya kusindika korosho vinakabiliwa na kitisho cha kufungwa kutokana na uuzaji mkubwa wa korosho ghafi nchini China. Jitihada za kudhibiti sekta ya viwanda kama vile kupiga marufuku uuzaji wa magogo kutoka Gabon na Msumbiji zimegonga mwamba. Nchini Gabon ambako China iliipiku Ufaransa kuhusiana na bishara ya magogo, karibu asilimia 60 ya mbao husafirishwa kwa njia za haramu kwenda nchini China.

Bango lililokuwa likitangaza mkutano wa kilele kati ya China na Afrika mjini Beijing.
Bango lililokuwa likitangaza mkutano wa kilele kati ya China na Afrika mjini Beijing.Picha: AP

Gavana wa benki kuu yay Nigeria anaeheshimika Lamidu Sanusi, alisema mwezi Machi kuwa uchukuaji wa rasilimali za Afrika unaofanywa na China, una kila sifa ya ukoloni. Katika kujaribu kutuliza wasiwasi wa Afrika, rais wa China Xi Jinping alitumia ziara yake ya siku sita barani humo kusisitiza kuwa China inatafuta ushirikiano unaotoa ushindi kwa pande zote.

Katika kujibu malalamiko ya baadhi ya serikali za Afrika, wizara ya Biashara ya China imezihamasisha kampuni kuongeza uwekezaji barani Afrika, na nchi hiyo imeanzisha kanda maalumu za kiuchumi kwa ajili ya makampuni yanayotaka kuwekeza barani humo. Ingawa ndiyo mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika, China ina asilimia 6 tu ya akiba ya uwekezaji wa kigeni, ikiwa nyuma sana ya Ufaransa yenye asilimia 18 kwa mujibu wa shirika la biashara la Umoja wa Maataifa UNCTAD.

Mwandishi: Iddi Ismail Ssessanga/rtre
Mhariri: Yusuf Saumu