CHILE. Idadi ya watu waliokufa yaongezeka baada ya tetemeko la ardhi
15 Juni 2005Matangazo
Idadi ya watu waliokufa kufuatia tetemeko la ardhi nchini Chile imeongezeka kufikia watu 11.
Tetemeko la ardhi lenye kipimo cha rishta 7.9 lilikumba sehemu ya kaskazini mwa Chile na kusababisha vifo huku wakaazi wa miji ya Arica, Iquique na Antofagasta wamekumbwa na uhaba wa nguvu za umeme na maji.
Utawala wa Chile umesema kuwa tetemeko hilo limefika hadi Bolivia na Peru.