1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chelsea kujiweka vizuri kunyakua Ligi

Sekione Kitojo
8 Mei 2017

Katika ligi ya England, viongozi  Chelsea wamefanya vizuri sana msimu huu na kuweza kubakia mbele ya mahasimu wao  wakubwa msimu huu Tottenham katika mbio za kuwania ubingwa wa ligi, amesema kocha Antonio Conte.

https://p.dw.com/p/2ccuY
Chelsea gegen Liverpool
Wachezaji wa Chelsea wakipambana na Liverpool katika Premeir LeaguePicha: Getty Images/AFP/I. Kington

Chelsea  wana nafasi  kubwa  ya  kushinda  taji  hilo na  wanaweza kupanua  mwanya  wa  uongozi  dhidi  ya  Tottenham  iliyoko  katika nafasi  ya  pili , baada  ya  kushindwa   kuidhibiti Leicester  City msimu  uliopita , na  kupanua  mwanya  hadi   pointi  saba  ikibakia michezo  mitatu iwapo  watashinda  mchezo  wao  leo  Jumatatu dhidi  ya  Middlesbrough  uwanjani  Stamford  Bridge.

Wakati   huo  huo  Jose  Mourinho  kocha  mkuu  wa  Manchester United  amesema  kipigo  cha  mabao  2-0  dhidi  ya  Arsenal London  kina  maana  itakuwa  vigumu  sana  kwa  timu  hiyo kunyakua  moja  kati  ya  nafasi  za  timu  nne  zinazoweza  kucheza katika  Champions League msimu  ujao.

Fußball - FA Cup  Manchester United gegen Wigan Athletic Bastian Schweinsteiger
Mchezaji Wayne Rooney akifurahi na mchezaji mwenzake wa zamani Bastian Schweinsteiger ambaye amehamia katika ligi ya MarekaniPicha: picture alliance/S. Stacpoole/Offside

Man United  ambayo  iko  katika  nafasi  ya  5 pointi  nne  nyuma  ya timu  iliyoko  katika  nafasi  ya  nne jirani  yake  Manchester  City ikibakia  michezo  mitatu  kumaliza  msimu , imebakiza  pia  mchezo dhidi  ya  Tottenham Hotspurs  unaoonekana  kuwa  mgumu  kwa timu  hiyo.

Katika  ligi  ya  Uhispania  La  Liga, Real Madrid  na  Barcelona zinaendelea  kukabana  koo  juu  ya  kilele  cha  ligi  hiyo  baada  ya kuwazaba  Granada  na  Villarreal  ugenini  kwa  vipigo  vya  mabao manne siku  ya  Jumamosi.

Champions League Real Madrid v Atletico Madrid
Wachezaji wa Real Madrid wakifurahia bao katika La LigaPicha: Reuters/S. Vera

Hata   hivyo  katika  ligi  hiyo  kulikuwa  na  mambo  mengine  lukuki ya  kutatuliwa   kukibakia  michezo  miwili  msimu  kufikia  mwisho.

Hakuna  mchezaji  barani  Ulaya  anayetakiwa  na  timu nyingine mbali  mbali  kama  Theo Hernandez. Kijana  huyo  Mfaransa mwenye  umri  wa  miaka  19  amekuwa  katika  klabu  ya  Alaves kwa  mkopo  kutoka  Atletico  Madrid , lakini  huenda  asirejee Atletico , lakini  huenda  akawa  katika  kikosi  cha  Real  ama barcelona , kwa  kuwa  timu  zote  zimekubali  kutoa  donge  la  euro milioni  24  kumpata  mchezaji  huyo  wa  ulinzi.

 

Mwandishi: Sekione  Kitojo / afpe / rtre / dpae

Mhariri: Josephat Charo