Mazungumzo ya kusaka suluhu ya mkwamo wa kisiasa ya ukumbi wa Bomas of Kenya yamepata kikwazo kipya. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Wafula Chebukati na wenzake watatu ambao hawakujiuzulu kabla ya uchaguzi mkuu kukamilika wamekataa kufika mbele ya kamati hiyo ya pande mbili kujieleza. Sikiliza ripoti ya mwandishi wetu wa mjini Nairobi, Thelma Mwadzaya.