1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chavez atofautiana na Uribe wa Colombia.

26 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CTGF

Caracas. Rais wa Venezuela Hugo Chavez amesema kuwa anasitisha uhusiano na serikali ya Colombia baada ya rais wa hiyo Avaro Uribe kumuondoa katika jukumu lake kama mpatanishi na waasi wa kundi la FARC. Chavez ametoa matamshi hayo katika hotuba iliyotangazwa na televisheni ya taifa. Amekuwa akijadiliana kuhusu kubadilishana wafungwa na kundi hilo la wapiganaji wa mrengo wa shoto nchini Colombia, lakini aliondolewa katika wadhifa huo baada ya kuzungumza moja kwa moja na kiongozi wa jeshi la Colombia. Hilo ni suala ambalo rais Uribe alimwambia asifanye. Rais wa Colombia amejibu taarifa ya Chavez kwa kumshutumu kutaka kuweka serikali ya waasi wa kundi la FARC mjini Bogota, kama sehemu ya mkakati wake wa kusambaza tawala za mrengo wa shoto katika eneo la Latin Amerika.