Ngozi Okonjo-Iweala ni msomi, mchumi na mtaalamu wa masuala ya fedha ya kimataifa na maendeleo, ameteuliwa kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya mkuu wa shirika la biashara la kimataifa WTO. Anachukuliwa kuwa mzungumzaji mwenye ujuzi wa kushawishi na kupata makubaliano. Je changamoto zipi zitakazomkabili? Sikiliza tathmini ya wachambuzi kwenye kipindi cha Maoni. Nahodha ni Josephat Charo