Kwa uchumi wa nchi yoyote ile kukua, ni lazima kuwepo na watu walioko tayari kuwekeza. Kwa hilo kufanikiwa, sharti pawepo na mazingira ya kuwavutia wawekezaji hao. Vipi kuhusu Tanzania? Kwanini kiwango cha uwekezaji bado kiko chini? Ni moja ya maswali tunayomuuliza Geoffrey Mwambe, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (Tanzania Investment Centre) TIC katika Kinagaubaga.