1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

​​​​​​​Champions league yaanza kutifua vumbi

11 Septemba 2017

Michuano ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inaanza wiki hii ambapo miamba wa Ujerumani Bayern na Dortmund wanakabiliwa na wapinzani wakali. RB Leipzig pia inajitosa katika dimba hilo kwa mara ya kwanza

https://p.dw.com/p/2jjOr
Fußball | Maulkorb für Thomas Müller
Picha: picture-alliance/dpa/A. Gebert

Real Madrid inalenga kushinda dimba hilo hilo kubwa barani Ulaya kwa mwaka wa tatu mfululizo, kitu ambacho hakijawahi kutokea tangu Bayern Munich katika miaka ya sabini.

Real watapambana na Apoel Nicosia, mabingwa wa Cyprus siku ya Jumatano. Mahasimu wao wa Uhispania Barcelona na makamu bingwa wa msimu uliopita Juventus wataangushana kesho. Bayern watacheza dhidi ya Anderlecht hiyo kesho.

Mabwenyenye wanaofadhiliwa na kampuni za Qatar Paris Saint Germain wa Ufaransa watakwaruzana na Celtic kesho, wakati siku ya Jumatano, Manchester City watakutana na Feyenoord.

Wakati huo huo, Manchester United, wanacheza nyumbani dhidi ya Basel, wakati Chelsea wakiwaalika wageni Qarabag wa Azerbaijan. Liverpool baada ya kuwa nje ya Champions League kwa miaka mitatu, watachuana na Sevilla uwanjani Anfield.

Kwingineko, RB Leipzig wanajitosa katika dimba hilo kwa mara ya kwanza kwa mtanange dhidi ya Monaco, wakati Tottenham Hotspur wakiwakaribisha Borussia Dortmund uwanjani Wembley. Porto watacheza dhidi ya Besiktas ya Uturuki. Roma watakwaruzana na Atletico Madrid. Napoli watakuwa wageni wa Shakhtar Donetsk.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP
Mhariri: Yusuf Saumu