Uhondo wa mechi za ligi ya mabingwa wa Ulaya, Champions League unarejea wiki hii. Kesho Jumanne Borussia Dortmund wanawakaribisha mabingwa wa ligi hiyo Real Madrid, wakitumai kuendeleza rekodi nzuri katika uwanja wa nyumbani. Dortmund watahitaji matokeo mazuri dhidi ya Real Madrid, hususan baada ya kichapo cha magoli 3-1 walichokipata kutoka kwa Tottenham mjini London majuma mawili yaliyopita. Katika mechi nyingine ya kundi H linalochukuliwa kama ''la kifo'' msimu huu, Tottenham itakuwa mgeni wa Apoel Nicosia katika uwanja wa GSP mjini Nicosia kisiwani Cyprus. Baadhi ya mechi nyingine za Champions League hapo kesho, Leipzig itaipokea Beskitas ya Uturuki, Manchester City itaikaribisha Shakhtar Donestk ya Ukraine, nayo Liverpool ya Uingereza itafunga safari hadi Urusi, kupambana na Spartak Moscow. Zaidi, sikiliza makala hii.