Chama tawala Zimbabwe chashindwa kudhibiti bunge
26 Aprili 2008Matokeo yaliotolewa leo hii yanaonyesha kushindwa kwa chama hicho tawala cha ZANU- PF kwa mara ya kwanza kabisa katika historia yake ya miaka 28 Mugabe alishinikiza kuhesabiwa upya kwa kura baada ya chama cha upinzani cha MDC kushinda wingi wa viti bungeni katika uchaguzi huo.Chama cha ZANU- PF kimekuwa kikiwashutumu maafisa wa uchaguzi kwa kupokea hongo ili kushusha idadi ya kura za chama hicho.
Kiongozi wa chama cha upinzani MDC Morgan Tsvangirai akiungwa mkono na Marekani amekuwa akidai kwamba ameshinda uchaguzi huo moja kwa moja ukiwemo ule wa rais ambao matokeo yake hadi hivi sasa hayakutangazwa.
Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe ZEC imesema kwamba majimbo 14 kati ya 23 kura zake zilizohesabiwa upya hadi sasa matokeo ya awali yamethibitishwa kuwa sahihi.
Suala la uchaguzi wa Zimbabwe linatazamiwa kujadiliwa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo Ijumanne ijayo..