1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTogo

Togo: Chama tawala chashinda uchaguzi wa Bunge

5 Mei 2024

Tume ya Uchaguzi nchini Togo imetangaza kuwa chama tawala cha rais Faure Gnassingbe cha UNIR kimepata ushindi katika uchaguzi wa Bunge kwa kujinyakulia viti 108 kati 113, hii ikiwa ni kulingana na matokeo ya muda.

https://p.dw.com/p/4fWC8
Rais wa Togo Faure Gnassingbe
Rais wa Togo Faure Gnassingbe Picha: Kola Sulaimon/AFP

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Dago Yabre amesema kiwango cha watu walioshiriki katika uchaguzi huo kilifikia asilimia 61.

Wakosoaji wanasema hatua hii huenda ikampa nafasi Rais Gnassingbe ambaye ameiongoza Togo kwa miaka 19, kuongeza muda wake madarakani baada ya kufanya marekebisho ya katiba na hivyo  kudumisha utawala wa kiimla.

Gnassingbe alimrithi babake Gnassingbe Eyadema, ambaye alitawala kwa takriban miongo minne nchi hiyo ndogo ya pwani ya Afrika Magharibi kati ya Benin na Ghana.