Chama tawala Georgia chaishtumu Marekani kwa kutumia vitisho
25 Mei 2024Rasimu ya sheria hiyo imesababisha mzozo wa kisiasa katika taifa hilo la kaukasusi ya kusini, ambapo waandamanaji wameingia mitaani katika baadhi ya maandamano makubwa zaidi tangu Georgia ilipopata uhuru wake kutoka iliyokuwa Jamhuri ya Kisovieti, kupinga muswada huo, ambao umelaaniwa pia na wakosoaji wa ndani, Marekani na Umoja wa Ulaya kuwa wa kiimla na ulioshawishiwa na Urusi.
Soma pia: Maandamano yanayopinga kubanwa kwa uhuru wa habari Georgia
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alisema siku ya Alhamisi kuwa Marekani inaweka vikwazo vipya vya viza dhidi ya Georgia na kuanzisha mchakato wa kupitia upya ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili kuhusiana na muswada huo, ambao utayataka mashirika yanayopokea zaidi ya asilimia 20 ya ufhadhili wake kutoka nje kujisali kama "mawakala wa kigeni."