Chama cha waziri mkuu wa Ethiopia kimeshinda uchaguzi mkuu na kujikusanyia jumla ya viti 237 vya bunge
6 Septemba 2005Matangazo
Muungano wa vyama tawala nchini Ethiopia unaoongozwa na waziri mkuu Meles Zenawi,umeshinda uchaguzi mkuu wa mwezi May uliopita.Baada ya miezi minne ya kuhesabu kura,kamisheni kuu ya uchaguzi imetangaza matokeo ya mwisho rasmi kwa viti vyote isipokua viwili tuu vya bunge la shirikisho la Ethiopia.Chama cha Waziri mkuu Meles Zenawi kimejikingia viti 327.Madai ya udanganyifu yaalizusha machafuko ambapo watu wasiopungua 36 waliouliwa na jeshi mwezi June uliopita.Bunge jipya la Ethiopia linatazamiwa kukutana mwishoni mwa mwezi huu kumteuwa waziri mkuu,anaetazamiwa kuwa Meles Zenawi mwenyewe.