1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha SPD kimeshinda uchaguzi wa Jimbo la Berlin

Martin,Prema/zpr19 Septemba 2011

Ujerumani, chama cha SPD kimeshinda uchaguzi wa jimbo la Berlin baada ya kujinyakulia asilimia 28. 3 ya kura zilizopigwa Jumapili.

https://p.dw.com/p/RmSA
Spitzenkandidat Klaus Wowereit (SPD) zeigt sich am Sonntag (18.09.2011) in Berlin bei der Wahlparty der SPD in der Kulturbrauerei zusammen mit seinem Lebensgefährten Jörn Kubicki seinen Anhängern. Rund 2,47 Millionen Berliner waren zur Wahl des 17. Berliner Abgeordnetenhauses aufgerufen. Foto: Bernd von Jutrczenka dpa/lbn
Mshindi wa chama cha SPD Klaus Wowereit (kati)Picha: picture-alliance/dpa

Chama cha CDU kimepata asilimia 23.4 na chama cha Kijani asilimia 17.6 - hayo ni matokeo mazuri kabisa kwa chama hicho katika mji mkuu Berlin. Chama cha mrengo wa kushoto Die Linke, kilichoshirikiana na SPD katika serikali ya mseto ya jimbo la Berlin, kimeangukia asilimia 11.7 tu. Kwa hivyo, SPD cha meya wa hivi sasa, Klaus Wowerweit, kitapaswa kutafuta mshirika mpya. Chama hicho kinaweza kuunda serikali ya jimbo la Berlin, kwa kushirikiana na chama cha Kijani au CDU.

Kwa mara ya kwanza kabisa, chama cha Die Piraten, kitawasilishwa katika bunge la jimbo, baada ya kupata asilimia 8.9 ya kura huku FDP kikipata pigo kubwa baada ya kuishia na asilimia 1.8 tu. Kwa hivyo,FDP kinachoshorikiana na chama cha CDU cha Kansela Angela Merkel katika serikali kuu, hakitokuwepo katika bunge la jimbo la Berlin.