1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha Mugabe cha ZANU PF chakutana

Kalyango Siraj4 Aprili 2008

Wandishi habari wa kigeni wawili wakamatwa kwa kutokuwa na kibali Zimbabwe

https://p.dw.com/p/Dc2W
Tendai Biti,Katibu mkuu wa chama cha Upinzani cha MDC nchini Zimbabwe akihutubia mkutano na waandishi wa habari Zimbabwe Harare,Jumatano, April, 2, 2008. Biti alitangaza kuwa namba walizokuwa nazo kutoka vituo mbalimbali vya kupigia kura zilionesha kuwa MDC imeshinda uchaguzi wa UraisPicha: AP

Mkutano wa chama tawala cha ZANU PF nchini Zimbabwe unaofanyika leo Ijumaa,huenda ukajadilia mikakati ya kujiandaa kwa duru ya pili ya uchaguzi wa urais ingawa matokeo rasmi hayajatangaazwa.Kwa upande mwingine chama cha upinzani kinadia kuwa kimeshinda .Kwa mda huohuo chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change MDC kimekanusha madai ya vyombo vya habari kuwa mmoja wa maafisa wake wa juu amekamatwa na polisi.

Ikiwa inasubiriwa kitakachotokana na mkutano mkuu wa chama cha Bw Robert Mugabe cha ZANU PF ambao umeitshwa leo kuhusu uchaguzi wa urais baado matokeo ya uchaguzi huo hayajatangazwa rasmi licha ya upande wa upinzani kudai kuwa ndio umeshinda.

Madai ya ushindi yanapingwa na chama cha ZANU PF kinachoashiria kuwa huenda kuna duru ya pili kutokana na matamshi ya waziri mdogo wa habari Bright Matonga.

Ikiwa tume ya uchaguzi itatangaza matokeo na kusema kuwa hakuna aliepata kile kiwango cha kuepuka duru ya pili,duru ya pili inapaswa kufanyika katika kipindi cha siku 21.Lakini upinzani kupitia Jameson Timba, bingwa wa masuala ya sheria wa chama cha MDC,unadai kuwa ZANU PF inapanga kupendekeza kuwa hali ya duru ya pili ikitokea eti wanataka ufanyike baada ya siku 90 yaani miezi mitatu.

Lakini hayo yote ni hadi matokeo kutangazwa na tume ya uchaguzi pamoja na kujua yaliyojiri kwenye mkutano wa chama cha ZANU PF ambapo kufikia sasa hatujapata habari zozote kuuhusu.

Kwa mda huohuo chama cha MDC kimekanusha habari ambazo zilikuwa zimezaga kuwa katibu wake mkuu amekamatwa na polisi katika kamatakamata walioifanya dhidi ya ofisi za chama hicho.Pia nalo hilo limekanushwa na msemaji wa MDC Nelson Chamisa katika mazungumzo ya simu na shirika la habari la Reuters.

Hata hivyo kuna waandishi habari wa kigeni wawili waliokamatwa.Habari za hivi sasa zinasema kuwa wamefikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa makosa ya kufanya kazi nchini bila kibali.