Raia wa Ureno wafanya uchaguzi wa mapema
10 Machi 2024Uchaguzi huo wa Ureno huenda ukaifanya nchi hiyo kujiunga na wimbi la mrengo wa kulia kote Ulaya baada ya miaka minane ya utawala wa Kisoshalisti. Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa saa mbili asubuhi katika taifa hilo lenye karibu watu milioni 10.
Wachambuzi wanaonya kuwa matokeo ya uchaguzi huo, ambao ni wa pili katika miaka miwili, bado yako wazi ikizingatiwa idadi kubwa ya wapiga kura ambao hawajaamua.
Uchunguzi wa mwisho wa maoni uliochapishwa Ijumaa ulionesha chama cha siasa za wastani za mrengo wa kulia cha Democratic Alliance - AD kikiwa mbele ya chama cha Kisoshalisti cha PS, kwa tofauti ya kura chache lakini kikipungukiwa na wingi wa viti bungeni.
Hiyo inaweza kukifanya chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Chega kuwa muhimu katika kuunda serikali ya muungano.