1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Chama cha Le Pen chashinda duru ya kwanza Ufaransa

1 Julai 2024

Chama cha siasa kali cha mrengo wa kulia nchini Ufaransa cha National Rally RN, kimepata mafanikio ya kihistoria kwa kushinda duru ya kwanza ya uchaguzi wa bunge uliofanyika siku ya Jumapili.

https://p.dw.com/p/4hjDR
Kiongozi wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha National Rally Marine Le Pen
Kiongozi wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha National Rally Marine Le PenPicha: Maillard/Maxppp/Imago

Kulingana na matokeo rasmi yaliyotangazwa na wizara ya mambo ya ndani mapema leo asubuhi, chama hicho cha siasa kali za  mrengo wa kulia cha National Rally kinachoongozwa na mwanasiasa maarufu nchini Ufaransa Marine Le Pen, kimepata asilimia 33 ya kura.

Soma pia:Ufaransa: Chama cha National Rally mguu sawa kuchukua hatamu 

Chama hicho kinafuatiwa na kundi la vyama vya mrengo wa kushoto lililojipatia asilimia 28 huku vyama vya siasa za wastani ikiwemo kile cha Rais Emmanuel Macron cha Muungano wa pamoja kikipata asilimia 20 tu ya kura. 

Hata hivyo iwapo maamuzi ya chama cha National Rally kuunda serikali yatategemea matokeo ya duru ya mwisho itakayofanyika wiki ijayo.