Dreikönigstreffen
6 Januari 2012Januari mwaka 2011 chama cha kiliberali cha FDP kilijiweka katika nafasi nzuri, ambapo kimekuwa mshirika wa serikali ya mseto katika upande wa chama cha kansela wa Ujerumani Angela Merkel, ambapo katika majimbo 16 ya hapa Ujerumani, chama hicho kinawakilishwa katika mabunge ya majimbo 15. Na kutokana na kupungua kwa umaarufu wa kiongozi wa wakati huo wa FDP Guido Westerwelle na kujikuta katika hali ngumu ya ukosoaji , alianza kutoa matamshi ya kujitetea, ambayo yalikuwa na lengo la kujiweka katika njia ya kukubalika tena. Lakini hilo halikuwezekana.
Mwaka mmoja baadaye chama hiki cha Kiliberali kinaangalia nyuma katika mwaka huo uliokuwa na mabonde na milima na hali ya kuogofya katika historia ya chama hicho.
Mwaka 2009 ulikuwa mbaya zaidi kama mshirika mkuu wa chama cha kihafidhina cha CDU/CSU, lakini hali hiyo ya mapenzi imeanza kupoa. Iwapo kutakuwa na uchaguzi wa mapema , FDP kwa uhakika kabisa inaweza kutupwa nje ya bunge la Ujerumani, Bundestag.
Itakuwaje , iwapo chama hicho kitatupwa nje ya bunge au kuwa chama cha upinzani nje ya bunge. Katika mwaka 2011 chama cha FDP kilitupwa nje ya bunge katika majimbo saba wakati wa uchaguzi wa majimbo hayo.
Rösler achukua nafasi ya Westerwelle kama mkuu wa chama.
Kuanguka kwa chama hicho katika ngazi ya majimbo kunakwenda sambamba na kiwango cha watendaji wenyewe. Waziri wa mambo ya kigeni mwanzoni mwa mwaka jana alilazimika kuachia ngazi na baada ya miaka kumi akiwa kiongozi wa chama hicho, ilibidi kumpa nafasi mtu mwingine kushika wadhifa wa mwenyekiti wa chama cha FDP. Baada ya kuteuliwa mridhi wake Mei mwaka 2011, Philipp Rösler alitaka kubadilisha hali hiyo ya kuporomoka. Rösler mwenye umri wa miaka 38 na ambaye ni tabibu alikuwa amebeba matumaini ya chama hicho. Lakini badala ya kuwa mtulivu na kutafakari , alijitambulisha kuwa kinyume cha mtangulizi wake Guido Westerwelle. Lakini wakati kunatakiwa kuwa na hali nyingine ya shauku katika chama hicho, FDP ilijikuta ikiangukia katika mkasa baada ya mkasa na kiongozi wao huyo mpya.
Hatua ngumu kabisa katika mporomoko huu, ilikuwa wakati alipojiuzulu katibu mkuu wa chama hicho Christian Lindner bila kutarajiwa.
Katibu mkuu mpya ateuliwa.
Kiongozi wa chama Philipp Rösler alichukua hatua haraka na kuwasilisha jina la Patrick Döring ambaye ni mshirika wake wa karibu, mwenye umri wa miaka 38 kijana kama yeye. Kwa kuwa naye Rösler anamatumaini kuwa chama cha FDP kinaweza tena kupambana . Hilo aliweza kuhisi kuwa linakosekana katika wakati wa Lindner kuwapo madarakani , anasema Döring. Anataka kuzungumzia kila kitu kwa uwazi , amesema Döring katika jarida la Stern. Mimi ni mzungumzaji mwenye ujuzi, na sio mtu wa kuzunguka zunguka na maneno , nasema wazi. Hii inaonekana kana kwamba ni hali ya kumsuta mtangulizi wake.
Kiongozi wa kundi la wabunge Brüderle anangojea nafasi yake.
Katika mkutano wao Januari 6 , 2012 hata hivyo hatakuwa na fursa. Kwa kuwa kama wazungumzaji , karibu na mtangulizi wa Brüderle katika wadhifa wa kiongozi wa wabunge wa FDP bungeni, yuko Birgit Homburger, waziri wa maendeleo Dirk Niebel, katibu mkuu Patrick Döring na hata mwenyekiti binafsi Philipp Rösler.Kutoka kwake inatarajiwa hotuba itakayoonyesha mwelekeo. Iwapo atafanikiwa , atakuwa amekiimarisha chama hadi Mei 6, ambapo kutakuwa na uchaguzi mpya wa jimbo katika jimbo la Schleswig - Holstein. Iwapo chama cha FDP kitaangukia katika upinzani nje ya bunge katika uchaguzi huo , hali ya baadaye ya chama hicho inaweza kuwa mbaya zaidi na kujikuta nje ya siasa za Ujerumani pamoja na mwakilishi wao ambaye pia ni waziri wa uchumi na makamu kansela Philipp Rösler.
Mwandishi : Marcel Fürstenau / DW Berlin / ZR / Sekione Kitojo
Mhariri : Othman Miraji