1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chad yaandaa Uchaguzi Mkuu

Lilian Mtono11 Aprili 2016

Raia wa Chad wamepiga kura kumchagua Rais, huku rais wa sasa Idriss Deby akiwania awamu ya tano, kwa kuahidi kuimarisha uthabiti wa serikali yake kukabiliana kitisho cha ugaidi kutoka kundi la wapiganaji la Boko Haram.

https://p.dw.com/p/1ITNV
Rais Idriss Deby
Rais Idriss DebyPicha: picture-alliance/dpa/E. Hamid/Ausschnitt

Kundi la wapiganaji la Boko limekwishafanya matukio ya mwendelezo ya ulipuaji wa mabomu nchini Chad katika miaka iliyopita, ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa kutanua uasi wa Kiislamu kutoka makao yake yaliyoko katika nchi jirani, eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

Chad ni miongoni mwa nchi zilizo na jeshi madhubuti Barani Afrika, na rais Deby amekuwa sehemu muhimu katika kutekeleza juhudi za kuliwezesha jeshi hilo akisaidiwa na nchi za Magharibi kukabiliana na kundi la Boko Haram lenye mahusiano makubwa na kundi la kigaidi la Dola la Kiislamu, IS na makundi mengine ya wapiganaji ya Kiislamu yenye mahusiano na Al Qaeda.

Washuhudiaji wanasema, maelfu ya wapiga kura kwenye mji mkuu wa nchi hiyo wamejitokeza kwenye vituo vyao, kwenye uchaguzi huo wa kwanza katika nchi za ukanda wa Afrika ya Kati kutumia mfumo wa Kielektroniki, Biometric Data, kupiga kura.

Deby ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1990, anaweza kukabiliana na duru ya pili ya uchaguzi kutokana na idadi kubwa ya wagombea. inatarajiwa kuwa moja ya uchaguzi mgumu kwake. Amesema Mchambuzi mwandamizi wa masuala ya kimataifa kutoka taasisi ya kimataifa inayoshughulikia mizozo, ICG, Thibaud Lesueur.

Kiongozi wa upinzani, Thibaud Lesuer
Kiongozi wa upinzani, Thibaud LesuerPicha: Getty Images/I. Sanogo

Raia wanataka mabadiliko ya kiuchumi.

Tume ya uchaguzi imesema inaweza kuchukua wiki kadhaa kwa matokeo kamili kutolewa. Rais Deby aliyeongoza waasi kushika madaraka mwaka 1990, anatarajiwa kuwashinda wagombea wengine 13, ambao ni pamoja na kiongozi wa upinzani Saleh Kebzabo anayepigia kelele sera ya mabadiliko nchini Chad.

Katiba ya Chad inamruhusu Deby kuwania tena, lakini rais huyo ameahidi kufanyia mabadiliko kikomo cha awamu kilichoondolewa na serikali yake mwaka 2004. Viongozi wengine barani Afrika wamekuwa wakijaribu kuondoa kipiengele hicho ili kujiongezea wigo wa utawala, hatua iliyosababisha machafuko katika nchi za Burundi, Burkina Faso na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Hali ya uchumi kwenye nchi hiyo isiyo na mpaka wa bahari, unategemea zaidi uzalishaji wa mafuta. Lakini kushuka kwa bei ya bidhaa hiyo kwenye soko la dunia, kumeyumbisha pato la serikali. Changamoto kubwa itakayoikumba serikali ijayo itakuwa ni kuangalia namna ya kuboresha hali ya uchumi kwa watu wake ambao wengi wanaishi katika hali ya umasikini.

Chad, ambayo ilikuwa koloni la zamani la Ufaransa hivi sasa ni makao ya operesheni za majeshi ya mtawala wake huyo wa zamani barani Afrika. Aidha, Wanajeshi wa Ufaransa ndio walio mstari wa mbele kwenye mapambano dhidi ya Boko Haram.