Ceuta:Wahamiaji wakiafrika wafariki wakijaribu kuingia Ceuta
29 Septemba 2005Matangazo
Watu 2 wamekufa katika jaribio la mamia ya wahamiaji wa kiafrika, la kuvuka mpaka baina ya Moroko na kisiwa kidogo cha kaskazini mwa Uhispania cha Ceuta. Vyombo vya habari vya Uhispania vimeripoti kwamba zilifyatuliwa risasi wakati wahamiaji wapatao 600 walipojaribu kupanda uzio wa senyenge mpakani kuingia Ceuta. Bado haijafahamika ni nani aliyefyatua riasasi hizo.Mnamo wiki chache zilizopita, maelfu ya waafrika wakitarajia kuingia katika ardhi ya Ulaya walijaribu mara kadhaa kuvuka na kuingia katika visiwa viwili vya pwani ya kaskazini mwa Afrika ambavyo ni mamlaka ya Uhispania-CEUTA na MELILLA. Maafisa wa serikali za Uhispania na Moroko watakutana baadae leo kulijadili suala hilo.