1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Casablanca, Morocco. Mtu mmoja ajilipua Morocco.

12 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJv

Polisi nchini Morocco wanachunguza iwapo mlipuko uliotokea usiku katika duka ambalo watu hupata huduma ya mtandao wa Internet ulikuwa ni shambulio la kujitoa muhanga.

Watu walioshuhudia wamesema kuwa mtu mmoja ambaye aliingia katika duka hilo na kuwa na mabishano na mmiliki wa duka hilo alilipua milipuko ambayo ilikuwa imefichwa katika nguo zake, na kujiua yeye mwenye na kuwajeruhi watu wengine wanne.

Mlipuko huo ulitokea katika eneo la kitongoji cha mji wa Casablanca cha Sidi Moumen, ambako watu 13 waliojitoa muhanga wanatoka , ambao wameuwa watu 32 mjini Casablanca katika mwaka 2003.

Jumapili ilikuwa siku ya kumbukumbu ya shambulio dhidi ya kituo cha treni mjini Madrid ambapo watu 191 waliuwawa.