CARACAS: Rais Chavez amechaguliwa tena kuiongoza Venezuela
4 Desemba 2006Matangazo
Rais wa Venezuela Hugo Chavez amechaguliwa kubakia madarakani kwa awamu nyingine ya miaka sita.Matokeo ya mwanzo ya uchaguzi uliofanywa siku ya Jumapili,yanaonyesha kuwa Hugo amepata asili mia 61 ya kura zilizohesabiwa.Kwa upande mwingine,mpinzani mkuu wa Chavez, Manuel Rosales,amejikingia asili mia 38 na amekubali kuwa ameshindwa.Wakati wa kampeni za uchaguzi,Rosales alimtuhumu Chavez kuwa anataka kuanzisha utawala wa mtu mmoja.Chavez anadhamiria kufanya mageuzi ya katiba,ikiwa ni pamoja na kuondosha vikwazo vinavyohusika na idadi ya awamu zinazorihusiwa ili kuweza kubakia madarakani kama rais.Mageuzi hayo yatamruhusu Chavez kugombea uchaguzi mara nyingine,hapo awamu yake ya pili itakapomalizika.