1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CANNES : Bashir akataa tena kikosi cha kimataifa

17 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCRV

Rais Omar al Bashir wa Sudan ameukataa wito wa karibuni kabisa kwa serikali yake kuruhusu uwekaji wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa katika jimbo lake la magharibi la Dafur.

Bashir alikuwa akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari mwishoni mwa mkutano wa siku mbili wa viongozi uliowakutanisha zaidi ya viongozi 30 wa Afrika katika mji wa Cannes nchini Ufaransa.Rais Jaques Chirac wa Ufaransa aliufunguwa mkutano huo kwa kuisihi Sudan kukubali kikosi hicho cha kulinda amani cha kimataifa.

Takriban watu 200,000 inaaminika kuwa wameuwawa na wengine zaidi ya milioni mbili wamelazimika kukimbia makaazi yao tokea kuzuka kwa mapigano hapo mwaka 2003 huko Dafur kati ya waasi na wanamgambo wa Janjaweed wanaoungwa mkono na serikali ya Sudan.