CANBERRA: Siasa kuhusu wakimbizi yabadilishwa
18 Juni 2005
Australia imeregeza siasa yake iliyozusha mabishano ya kuwatia ndani moja kwa moja wakimbizi wanaoingia Australia kwa njia zisizo halali.Waziri mkuu John Howard amelazimika kubadilisha msimamo wake,baada ya wanachama wenzake katika serikali yake kutishia kuwa watakwenda upande wa upinzani,wakilalamika dhidi ya kile walichokieleza kuwa ni utaratibu usio na huruma.Badiliko kubwa lililofanywa ni kuwa familia zenye watoto,sasa zitapelekwa katika jamii badala ya kuwekwa kizuizini kwenye vituo maalum.Miongoni mwa mageuzi mengine ni kuharakisha utaratibu wa ukaguzi wa maombi ya ukimbizi.Nchini Australia,tawi la shirika la Amnesty International linalopigania haki za binadamu duniani,limefurahia mageuzi hayo,lakini kwa wakati huo huo limesisitiza kuwa bado kuna mambo yanayotia shaka.