1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

“Campeo11es!" Real washerehekea Madrid

30 Mei 2016

Mji wa Madrid ulikuwa na wikendi yenye hisia nyingi, ambapo upande mmoja ulikuwa na furaha na mwingine ukawa na huzuni. Real Madrid ilinyakua kombe lake la 11 la Ulaya kwa kuipuku Atletico Madrid mjini San Siro

https://p.dw.com/p/1IxIN
UEFA Champions League Real Madrid Siegesfeier
Picha: picture-alliance/dpa/V. Lerena

Na kuanzia Jumamosi usiku, hadi kufikia jana mchana, MADRID ambayo inajiita kuwa ni mji mkuu wa kandanda duniani ilifurika hadi pomoni kuwakaribisha nyumbani mashujaa wao Real Madrid pamoja na kombe lao la 11 la Ulaya.

Mshindi mara tatu wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka duniani Cristiano Ronaldo ambaye alifunga penalti ya ushindi iliyoipa Real ushindi dhidi ya watani wao wa Atletico aliwashukuru mashabiki "Bila msaada wenu hatungeshinda kombe hili marisdadi tulilonalo hapa. Nnahisi fahari kubwa kuvaa jezi hii nyeupe inayonifaa kabisa. Nna furaha sana. Nilikuwa na maneno lakini pia ningependa niimbe. Real Madrid hushinda hivi, Real Madrid hushinda hivi! Ndiyo!

Ilikuwa mara ya pili katika miaka mitatu ambapo Real iliishinda Atletico katika fainali ya Champions League.

Madrid, mji mkuu wa Uhispania wenye jumla ya wakaazi milioni 3.2 ulitawaliwa na nembo na rangi za jezi za timu zote mbili kabla ya fainali hiyo iliyochezwa uwanjani San Siro, Italia, na iliyowavutumia watazamaji milioni 180 katika zaidi ya nchi 200.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Mohammed Khelef