Cameroon kucheza katika Kombe la Dunia
18 Novemba 2013Timu hizo mbili zilitoka sare ya bila kufungana katika mkondo wa kwanza nchini Tunisia. Sasa The Indomitable Lions wanaungana na Nigeria na Cote d'Ivoire ambazo zilishinda mechi zao za mchujo hapo Jumamosi, na kufungasha virago kuelekea Brazil. Cote d'Ivoire walitoka sare ya kufungana goli moja kwa moja dhidi ya Senegal ambalo na hivyo ikafuzu kwa jumla ya magoli manne kwa mawili mjini Casablanca, Morocco.
Mapema, The Super Eagles, walifuzu kwa mara ya tano katika tamasha hilo baada ya kuwapiku Ethiopia mabao mawili kwa sifuri nyumbani Calabar, na hivyo kupata jumlaya magoli manne kwamoja.
Timu mbili za Afrika zilizobaki zitajulikana hapo kesho Jumanne, wakati Misri ikihitaji muujiza mkubwa katika kujaribu kubatilisha kichapo cha mkondo wa kwanza cha magoli sita kwa moja dhidi ya Ghana.
Lakini vita vikali vitakuwa katika mchuano kati ya wenyeji Algeria na Burkina Faso katika uga wa Mustapha Tchaker mjini Blida, ambako Algeria haijawahi kupoteza katika michuano 19 tangu mwaka wa 2002. Burkina Faso wana faida ya magoli matatu kwa mawili kutokana na mkondo wa kwanza.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri:Yusuf Saumu