1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAIRO: Waislamu waitaka Marekani iombe msamaha

28 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CF9L

Kwa maelfu watu katika nchi za kiislamu wamefanya maandamano dhidi ya madai kuwa katika kituo cha kijeshi cha Marekani,Guantanamo Bay,Koran takatifu ilikufuriwa. Wafanya maandamano nchini Misri,Pakistan,Jordan,Lebanon na Malaysia wanaitaka serikali ya Marekani iombe radhi na wale waliohusika na kitendo hicho waadhibiwe.Maandamano hayo yamefanywa baada ya jeshi la Marekani kukiri kuwa baadhi ya walinzi wake wamefanya vitendo visivyostahilika kuhusu kitabu takatifu cha Koran,lakini walikataa kuwa kitabu cha Koran kilitumbukizwa chooni.Hapo awali ripoti ya jarida la Marekani,Newsweek kuwa kitabu takatifu cha Koran kilitumbukizwa chooni,ilizusha maandamano katika eneo la Mashariki ya Kati.Nchini Afghanistan katika machafuko yaliotokea si chini ya watu 15 walipoteza maisha yao.