CAIRO: Misri kujenga mitambo ya nyuklia
29 Oktoba 2007Matangazo
Rais Hosni Mubarak wa Misri ametangaza miradi ya kujenga mitambo kadhaa ya nyuklia kwa matumizi ya amani.Amesema,mtambo wa kwanza wa nyuklia utajengwa kwa kushirikiana na Shirika la Nishati ya Nyuklia la Umoja wa Mataifa IAEA.
Wakati huo huo,Rais Mubarak alisisitiza kuwa Misri itaheshimu mkataba unaozuia uenezaji wa silaha za nyuklia.Akaongezea kuwa ifikapo mwaka 2020,Misri inatazamia kuzalisha asilimia 20 ya nishati yake,kwa kutumia upepo na jua.Misri ilianzisha mradi wa kinyuklia katika miaka ya 70 lakini ulisitishwa baada ya kutokea ajali kwenye mtambo wa nyuklia wa Chernobyl katika Ukraine mwaka 1986.