Burundi yadai Rwanda inawasaidia waasi
12 Mei 2024Wizara ya mambo ya ndani imesema kuwa waasi wa kundi la RED-Tabara wanaoshutumiwa kwa msururu wa mashambulizi nchini Burundi kwa usaidizi waRwanda, walirusha guruneti kwenye kituo cha mabasi kilichokuwa kimejaa watu katika mji mkuu Bujumbura siku ya Ijumaa jioni.
Soma pia:Watu 8 wauawa, kadhaa wajeruhiwa Burundi
Msemaji wa wizara hiyo Pierre Nkurikiye amethibitisha kujeruhiwa kwa watu hao 38 na kusema hakuna vifo vilivyoripotiwa, lakini duru za polisi na mashuhuda zimeliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba watu watatu waliuawa.
Burundi imekuwa ikiishtumu Rwanda kwa kuwafadhili waasi
Katika shambulio sambamba na hilo karibu na kituo cha mafuta wilayani Ngagara, Nkurikiye amesema ni mshambuliaji pekee aliyejeruhiwa na kukamatwa. Mara kwa mara, Burundi imekuwa ikiishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi hao, madai ambayo yamekanushwa na serikali ya Rwanda na kundi hilo la RED-Tabara.