1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBurkina Faso

Burkina Faso yaitaka Ufaransa kuondoa wanajeshi wake

23 Januari 2023

Serikali ya Burkina Faso imefafanua kuwa imeitaka Ufaransa kuwaondoa wanajeshi wake katika nchi hiyo inayozongwa na uasi wa itikadi kali ndani ya mwezi mmoja.

https://p.dw.com/p/4MbAh
Burkina Faso | Französische Armee
Picha: Michele Cattani/AFP/Getty Images

Ufaransa ina karibu wanajeshi 400 wa kikosi maalum wanaohudumu Burkina Faso, lakini mahusiano yamedorora katika miezi ya hivi karibuni.

Msemaji wa serikali ya kijeshi ya Burkina Jean-Emmanuel Ouedraogo amesema wanasitisha makubaliano yanayoviruhusu vikosi vya Ufaransa kuwa Burkina Faso

Ameongeza kuwa huo sio mwisho wa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Burkina Faso na Ufaransa. Ouedraogo amesema kusitishwa kwa mkataba huo ni hatua ya kawaida na kulikuwa sehemu ya masharti ya makubaliano hayo.

Amesema utawala wa kijeshi na nchi nzima wanataka kuwa wahusika wakuu katika kuyakomboa maeneo yaliyoangukia mikononi mwa wanamgambo wenye itikadi kali.