1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroBurkina Faso

Burkina Faso yasema makundi ya waasi yanawalenga raia

18 Januari 2023

Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso Kapteni Ibrahim Traore amesema mashambulizi ya makundi ya itikadi kali yameongezeka nchini humo tangu mwezi Oktoba, na hivi sasa yanawalenga zaidi raia.

https://p.dw.com/p/4MOBs
Burkina Faso | PK Ibrahim Traore
Picha: AA/picture alliance

Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso Kapteni Ibrahim Traoreamesema mashambulizi ya makundi ya itikadi kali yameongezeka nchini humo tangu mwezi Oktoba, na hivi sasa yanawalenga zaidi raia.

Akizungumza Jumanne siku chache baada ya wanawake 50 kuchukuliwa mateka, Kapteni Traore ameapa kuutokomeza uasi unalizonga eneo la kaskazini mwa Burkina Faso.

Traore aliyekuwa akiwahutubia wanafunzi mjini Ouagadougou amesema wanajeshi wamevalia njuga mapambano dhidi magaidi, ndio sababu wamewageukia raia wasio na hatia, wakiwauwa na kuwadhalilisha.

Kapteni Traore mwenye umri wa miaka 34 alichukua hatamu za uongozi kupitia mapinduzi ya kijeshi ya Septemba 30 mwaka jana, akiiangusha serikali nyingine ya kijeshi iliyokuwa imeingia kwa njia hiyo hiyo ya mapinduzi.

Maelfu ya watu wameuawa katika ghasia zinazosababishwa na makundi ya kijihadi tangu yalipoingia nchini Burkina Faso yakitokea Mali.