1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Burkina Faso yachunguza madai ya mauaji ya watu wengi

Sylvia Mwehozi
28 Aprili 2024

Serikali ya Burkina Faso inachunguza mauaji ya watu wengi yanayodaiwa kufanywa mwezi Februari katika vijiji viwili vya Kaskazini mwa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4fGyX
Burkina Faso
Burkina FasoPicha: DW Akademie

Serikali ya Burkina Faso inachunguza mauaji ya watu wengi yanayodaiwa kufanywa mwezi Februari katika vijiji viwili vya Kaskazini mwa nchi hiyo. Hatua hiyo ni baada ya Shirika la Kimataifa la Haki za binadamu la Human Rights Watch kuripoti kwambajeshi la nchi hiyo liliwaua watu 223.

Hata hivyo msemaji wa serikali ya Burkina Faso Rimtalba Jean Emmanuel Ouedraogo amekanusha ripoti za shirika hilo alizozitaja kuwa ni uzushi na madai kwamba serikali ya kijeshi haikuwa tayari kufanya uchunguzi.

Ouedraogo ameongeza kwamba mauaji katika vijiji viwili vya Nodin na Soro tayari yameanza kuchunguzwa. Katika ripoti yake mapema wiki hii, Shirika la Human Rights Watch likinukuu mahojiano kwa njia ya simu na mashahidi, asasi za kiraia na wengine, lililishutumu jeshi la nchi hiyo kwa kuwaua watu 223, wakiwemo watoto 56.