Bunge limeahirisha kumchagua rais mpya Lebanon
20 Januari 2008Matangazo
BEIRUT: Bunge nchini Lebanon kwa mara ya 13 limeahirisha kupiga kura kumchagua rais mpya wa nchi hiyo.Rais wa bunge,Nabih Berri amesema,wabunge watakutana tarehe 11 mwezi Februari kumchagua rais mpya na sio siku ya Jumatatu,kinyume na ilivyopangwa hapo awali.
Tangu majuma kadhaa serikali ya Lebanon inayoelemea kambi ya Magharibi na upinzani unaoiunga mkono Syria,zinajadiliana kuhusu uchaguzi wa rais mpya.Muhula wa rais wa zamani Emile Lahoud ulimalizika mwisho wa mwezi Novemba na tangu wakati huo,Lebanon haina kiongozi wa taifa.