Bunge laidhinsha serikali mpya ya Somalia
11 Januari 2008BAIDOA
Bunge nchini Somalia hapo jana liliidhinisha baraza la mawaziri lililopendekezwa na waziri mkuu wakati mapigano yakiendelea nchini humo.Watu saba wameuwawa katika mapigano ya karibuni.Serikali ya Waziri mkuu Nur Hassan Hussein imekuwa ikikubwa na mvutano wa ndani wa kisiasa pamoja na kuongezeka kwa mashambulio ya waasi katika mji mkuu Mogadishu.Waziri mkuu Hussein alilitangaza baraza lake la mawaziri ijumaa iliyopita baada ya mivutano ya kikoo kuihujumu serikali iliyopita mwezi uliopita.Katika kura ya kuidhinisha baraza hilo,kwa mujibu wa spika wa bunge Aden Madobe,ni wabunge watano tu waliopinga kati ya 230.Waziri mkuu alitangaza mawaziri 15 tu badala ya 18 lakini spika wa bunge amesema mawaziri wengine watatangazwa hivi karibuni.