1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Umoja wa Ulaya latoa wito wa uchaguzi mpya Georgia

28 Novemba 2024

Bunge la Ulaya linataka uchaguzi mpya ufanyike nchini Georgia. Bunge hilo limeuhimiza Umoja wa Ulaya kuwawekea vikwazo viongozi wa Georgia baada ya uchaguzi wenye utata uliokumbwa na kasoro nyingi.

https://p.dw.com/p/4nXGf
 Georgia
Baadhi ya wanaharakati wanaopinga uchaguzi Georgia Picha: Alexander Patrin/TASS/IMAGO

Wabunge hao wamepitisha kwa wingi azimio linalokilaumu chama tawala nchini Georgia cha Georgian Dream kwa kufanya uchaguzi mwezi uliopita ambao walisema haukuwa wa huru na haki. Georgia, ambayo ni jamhuri ya zamani ya Kisovieti inawania kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya.

Lakini umoja huo wenye nchi 27 wanachama umesitisha mazungumzo, ukikituhumu chama cha Georgian Dream kwa kurudisha nyuma demokrasia na kuiondoa nchi hiyo kwenye mkondo wake wa kuegemea Magharibi na kuirejesha kwenye njia ya Urusi.

Tume ya uchaguzi yathibisha matokeo Georgia

Katika azimio lisilo na uzito wa kisheria, wabunge wa Ulaya wamesema uchaguzi wa Oktoba urudiwe ndani ya mwaka mmoja chini ya uangalizi mkali wa jamii ya kimataifa na taasisi huru ya uchaguzi.

Chama hicho kinakanusha tuhuma za udanganyifu katika uchaguzi. Wabunge wa upinzani wamesusia vikao vya bunge jipya.