1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Ujerumani lapitisha bajeti ya mwaka 2012

26 Novemba 2011

Wabunge wa Ujerumani wameridhia bajeti ya mwaka 2012, ambayo itakuwa na deni jipya la euro bilioni 26, ambalo ni kubwa kulinganisha na la mwaka 2011, lakini halihatarishi usalama wa kiuchumi wa taifa hili.

https://p.dw.com/p/13Hap
Kansela Angela Merkel (kati) akipanga foleni ya kupiga kura Bungeni kwa ajili ya bajeti.
Kansela Angela Merkel (kati) akipanga foleni ya kupiga kura Bungeni kwa ajili ya bajeti.Picha: dapd

Bajeti hiyo ya euro bilioni 306, imepitishwa kwa kura kutoka vyama vya mrengo wa kulia na kati, vya serikali ya mseto ya Kansela Angela Merkel, baada ya siku kadhaa za majadiliano Bungeni. Kiwango cha kukopa kitakuwa kikubwa kidogo, ikilinganishwa na kile cha euro bilioni 22, cha mwaka huu.

Waziri wa Fedha, Wolfgang Schäuble, amesema anatarajia nakisi ya bajeti ya mwaka ujao, itakuwa ya chini kidogo kuliko ya mwaka huu. Upinzani umemlaumu Kansela Merkel kwa kuongeza deni jipya, huku kiongozi huyo wa taifa kubwa kiuchumi Ulaya, akizihubiria serikali nyengine barani humu, kupunguza ukopaji ili kukabiliana na mgogoro wa madeni.

Mwandishi: Mohammed Khelef/ZPR 

Mhariri: Prema Martin