Bunge la Togo laidhinisha marekebisho ya katiba inayopingwa
20 Aprili 2024Wabunge kwa kauli moja waliidhinisha marekebisho yanayorefusha kipindi cha urais hadi miaka sita kutoka mitano, huku ukomo wa mihula ukiwa ni mmoja.
Chini ya katiba hiyo iliorekebishwa ambayo inaleta mfumo wa serikali ya bunge, rais hatachaguliwa tena na wananchi, badala yake wabunge watatekeleza mchakato huo.
Bunge lilipitisha marekebisho hayo katika kura iliopigwa mwezi Machi, lakini mashauriano zaidi na upigwaji kura awamu ya pili ulipangwa huku uchaguzi wa wabunge ukisogezwa kutokana na kukabiliwa na upinzani mkali.
soma pia:Upinzani Togo waitisha maandamano kupinga kuahirishwa uchaguzi wa Bunge
Wanao pinga mabadiliko hayo wanahofia kwamba wabunge wanaweza kuruhusu kurefushwa zaidi kwa utawala wa miaka 19 wa Rais Faure Gnassingbe na familia yake. Babayake na mtangulizi wake Gnassingbe Eyadema alinyakua mamlaka kupitia mapinduzi ya mwaka 1967.