Bunge la Tanzania lajiandaa kupitisha sheria ya watu wenye ulemavu
5 Mei 2009Matangazo
Serikali ya Tanzania imeaanda mswada wa sheria ya haki na maendeleo ya watu wenye ulemavu nchini humo. Mswada huo utawasilishwa bungeni na kujadiliwa kabla kupitishwa kuwa sheria itakayosaidia kuwalinda zaidi watu wenye ulemavu wa aina yoyote ile nchini Tanzania pamoja na kuboresha utoaji wa huduma msingi kwa watu hawa.
Sikiliza mahojiano kati ya Josephat Charo na mheshimwa Margaret Mkanga, mbunge viti maalum kundi la watu wenye ulemavu Tanzania, kuhusu mswada huo. Kwanza anaeleza hisia zake kuhusu mswada huo.