Bunge la Namibia lajadili maridhiano na Ujerumani
9 Juni 2021Kura hiyo inatarajiwa kupigwa siku chache zijazo, na kisha kusainiwa na mawaziri wa kigeni wa nchi zote mbili.
Waziri mkuu Saara Kuugongelwa aliwasilisha mpango wa makubaliano hayo na kueleza tathmini tofauti za umma kuhusu nakala hiyo, lakini akaongeza kwamba ni muhimu kuwa na umoja wa kitaifa.
soma zaidi: Maoni: Ujerumani yatambua mauaji ya halaiki ya enzi za wakoloni nchini Namibia
Zaidi ya miaka 100 baada ya Ujerumani kufanya uhalifu katika koloni lake ambalo sasa ni Namibia, serikali ya Ujerumani hatimaye iliyatambua mauaji yaliyofanywa dhidi ya jamii za Waherero na Wanama kuwa ya kimbari katika makubaliano hayo.
Ujerumani inakusudia kukiomba rasmi msamaha kizazi cha wahanga na imetenga euro bilioni 1.1 kuwasaidia kwa muda wa miaka 30 ijayo.