1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Bunge la Marekani laidhinisha msaada wa kijeshi kwa Israel

3 Novemba 2023

Bunge la Marekani limeidhinisha msaada wa kijeshi wa karibu dola bilioni 14.5 kwa Israel ambayo inaendelea na vita vyake dhidi ya kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/4YM4A
Bunge la Marekani limeidhinisha misaada zaidi ya kijeshi kwa Israel lakini sio kwa Ukraine. Rais Joe Biden anashauri Ukraine kupewa misaada zaidi katika kukabili uvamizi wa Urusi nchini humo.
Bunge la Marekani limeidhinisha misaada zaidi ya kijeshi kwa Israel lakini sio kwa Ukraine. Rais Joe Biden anashauri Ukraine kupewa misaada zaidi katika kukabili uvamizi wa Urusi nchini humo.Picha: Anna Moneymaker/Getty Images

Spika mpya wa Bunge hilo Mike Johnson amekaidi wito wa rais Joe Biden wa kuijumuisha Ukraine katika msaada huo.

Biden amesema atauzuia uamuzi huo kwa kura yake ya turufu.

Hata hivyo maafisa wa ngazi za juu mjini Washington wamebainisha Ijumaa kuwa Marekani inatarajia kutoa msaada mpya wa kijeshi wa dola milioni 425 kwa Ukraine, pamoja na kuipatia Kyiv silaha na vifaa vya kijeshi vyenye thamani ya dola milioni 125 ili kukabiliana na uvamizi wa Urusi.