Bunge la Kenya yaidhinisha polisi kutumwa nchini Haiti
16 Novemba 2023Bunge limeunga mkono mswada uliowasilishwa na Kamati ya bunge ya Utawala na Usalama wa Ndani na kuridhia ombi la serikali kuwatuma maafisa wa usalama nchini Haiti.
Kulikuwa na mjadala mkali bungeni huku wabunge wa upinzani wakiipinga mipango hiyo ya serikali, wakisema inakiuka katiba ya nchi.
Waliouunga mkono mswada huo walisema Kenya ina jukumu la kimaadili na wajibu wa kuisaidia Haiti.
Maswala muhimu katika mjadala huo yalikuwa ni nani atakayeufadhili ujumbe huo na sababu gani zinahalalisha kupelekwa kwa vikosi vya usalama Haiti, ambayo iko umbali wa maelfu ya kilomita kutoka Kenya.
Mahakama ya Juu mjini Nairobi inatarajiwa kutoa uamuzi dhidi ya kesi iliyowasilishwa na mgombea urais wa zamani Ekuru Aukot aliyehoji kuwa ujumbe huo, unaooungwa mkono na Umoja wa Mataifa, ni kosa na kuwatoa muhanga polisi wa Kenya.