1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Utawala wa sheriaIsrael

Bunge la Israel lapitisha sheria tata ya mageuzi ya mahakama

24 Julai 2023

Serikali ya misimamo mikali ya mrengo wa kulia ya Israel imepitisha kupitia kura ya bunge kipengele muhimu cha muswada wake wenye utata wa marekebisho ya mfumo wa mahakama.

https://p.dw.com/p/4UK71
Israels Parlament verabschiedet Gesetz zu Justizumbau
Picha: Maya Alleruzzo/AP/dpa/picture alliance

Hiyo ni licha ya miezi kadhaa ya maandamano ya umma na wasiwasi ulioonyeshwa na washirika wa kigeni.

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahuna washirika wake wa serikali ya muungano waliidhinisha mswada huo katika bunge la Knesset, kura iliyosusiwa na wabunge wa upinzani.

Wakosoaji wanahoji kuwa marekebisho hayo yatahujumu demokrasia ya kiliberali ya Israel kwa kuondoa uwezo wa kuidhibiti ofisi ya waziri mkuu.

Nayo serikali inahoji kuwa inahitaji kuidhibiti idara ya mahakama dhidi ya kuingilia utenda kazi wa serikali.

Soma pia:Maandamano dhidi ya serikali yatanda Israel

Mswada huo ambao umepitishwa kwa kura 64 katika bunge lenye viti 120, unalenga kuyapunguza mamlaka ya Mahakama ya Juu katika kuyabatilisha maamuzi ya serikali ambayo majaji wanayaona kama yasiyofaa.

Polisi tangu asubuhi walikabiliana na waandamanaji waliofurika nje ya bunge.