Bunge la Afrika Mashariki laanza vikao vyake Zanzibar
26 Februari 2019Bunge la Afrika Mashariki limeanza kikao chake cha wiki mbili Zanzibar, likiwa na ajenda kadhaa ikiwepo kulaani mashambulizi ya kigaidi yaliyotekelezwa hivi karibuni nchini Kenya.
Kwa mujibu wa Spika wa bunge hilo la Afrika mashariki Bw. Martin Ngonga, linalowajumuisha Kenya, Uganga, Burundi, Rwanda, Sudan ya Kusini na wenyeji Tanzania, ajenda zitakazojadiliwa ni kupambana na rushwa, utawala bora, ukuzaji wa lugha ya Kiswahili, usawa wa kijinsia na maswala ya watu wenye ulemavu.
Akizinduwa bunge hilo leo, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein alisisitiza juu wa nchi wanachama kuimarisha ushirikiano ili kutokomeza rushwa ambao imekuwa ikirudisha jithada za maendelo nyuma.
Aliwaambia wajumbe wa bunge hilo pamoja na waalikwa waliohudhuria katika uzinduzi wa bunge hilo kwamba Zanzibar pamoja na Tanzania bara zimekua na jithada kubwa kupambana na rushwa na jithanda hizo zimeonesha kuzaa matunda kutokana na baadhi ya watu kukamatwa na kufikishwa mahakamani.
Dkt. Shein alisema harakati za kukuza uchumi katika kila nchini wanachama zimekuwa zikiendelea vizuri ambapo ukuwaji wa uchumi umepanda kutoka asilimia 4.4 mwaka 2016 hadi asilimia 4.6 mwaka 2017.
Katika hotuba yake, rais wa Zanzibar pia alitoa wito kwa kuimarisha tecknonojia, miundombinu ya barabara, sambamba na kujenga viwanda ambavyo pia vitapunguza tatizo la ajira nchini.
Dk Shein pia alitumia fursa hiyo kutoa wito wa kuimarisha Kiswahili japo lugha iliyotumika leo na wasemaji wote walizungumza kiingereza.
Hii ni mara ya tatu Bunge la Afrika Mashariki kufanya mikutano yake Zanzibar ambapo katika kuwakaribisha, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Zubeir Ali Maulid alisema kufanyika kwa vikao vya bunge hilo hapa ni fursa ya kuimarisha ushirikiano pamoja kubadilishana uzoefu kati ya wajumbe wa baraza la wawakilishi wa wabunge wa bunge la Afrika Mashariki.
Mwandishi: Salma Said / Zanzibar
Mhariri: Sekione Kitojo