1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUNDESLIGA YARUDI LEO UWANJANI-RAIS WA IOC AZURU MECCA YA RIADHA-ELDORET-KENYA

20 Januari 2005
https://p.dw.com/p/CHZY
  • KOCHA WA UJERUMANI AWATEUA MICHAEL BALLACK NA OLIVER KAHN KATIKA TIMU YA UJERUMANI ITAKAYOPAMBANA NA TIMU YA MASTADI WA KIMATAIFA YA BUNDESLIGA KWA MCHNAGO WA TSUNAMI
  • -NA ENZI 4 ZA WANARIADHA WA KENYA ZAKUTANA NA RAIS WA IOC JACQUES ROGGE HUKO ELDORET.

Bundesliga-Ligi ya Ujerumani ilirudi uwanjani jana kwa mpambano kati ya viongozi wa Ligi-Bayern Munich na Hamburg katika Uwanja wa olimpik wa Munich.

Bayern munich baada ya kuanza vibaya msimu huu chini ya kocha mpyxa Felix Margath,iliparamia kileleni mwa Ligi ilipoenda likizoni kabla ya X-masi ikiongoza tu kwa magoli lakini pointi sawa na schalke.Munich ilifungua dimba jana na Hamburg na leo jumamosi kuna ajenda kamili ya Bundesliga mkabla ya kesho bayer Leverkusen kukutana na hannover na Bochum na Berlin.

Katika dakika za mwisho wakati huu, mabingwa brtemen wanaumana na Schalke; mainz imeikaribisha Stuttgart nyumbani na Borussia Mönchengladbach inatoana jasho na Armenia Bielefeld .Borussia Dortmund iliokumbwa na msukosuko inacheza na Wolfsburg.

Hansa Rostock-timu pekee katika daraja ya kwanza ya Bundeslioga kutoka mashariki mwa Ujerumani, inachezana freiburg.Kaiserslauten inakamilisha ajenda ya leo kwa changamoto na Nüremberg.

CHANGAMOTO YA DIMBA JUMAANE HII KUCHANGIA FEDHA KWA WEAHANGA WATSUNAMI:

Timu ya Taifa ya Ujerumani itapambana na ile ya mchanganyiko ya mastadi wa kimataifa wanaocheza katika Bundesliga ili kukusanya fedha kwa wahanga wa maafa ya Tsunami huko Asia:

Katika kikosi chake kwa changamoto hiyo, kocha wa Ujerumani Jürgen Klinsmann amewateua mastadi kama kipa Oliver Kahn na nahodha Michael Ballack.

Mpambano huo utachezwa katika uwanja maridadi wa Schalke mjini Gelsenkirche. Shirikisho la dimba la ujerumani latumai kukusanya hadi Euro milioni 3.5 mpaka milioni 4 kutoka mechi hiyo.

Kocha wa timu ya daraja ya pili ya FC Cologne, Huub Stevens ataiongoza timu ya kimataifa ya wachezaji wa Bundesliga.Kikosi chake kitajumuisha mastadi kama vile mshambulizi wa Bayern munich kutoka Holland Roy Makaay ,stadi wa kombe la dunia wa Brazil Lucio na mcheki Tomas Rosicky.

Chipukizi Christian Pander atavaa kwa mara ya kwanza jazi ya taifa upande wa Ujerumani.

KOMBE LA VIJANA LA AFRIKA LAENDELEA HUKO BENIN:

Kesho Angola inakumbana na Morocco na Misri na Lesotho katika mapambano ya kundi B.

Kati ya wiki hii, Lesotho ilitimua nje Angola kwa bao 2:1 wakati mabingwa Misri walimudu sare tu mabao 2:2 na Morocco.

Washindi wa kila kundi na wapili wataingia nusu-finali na baadae kukata tikiti ya kuiwakilisha Afrika katika Kombe la dunia la vijana chini ya umri wa miaka 17 nchini Holland hapo juni.

Kombe hili la vijana liligubikwa mwishoni mwa wiki iliopita kwa kuuliwa kipa wa timu ya Benin Yessouffo Semiou kwa kuwa tu Nigeria iliufumania mlango wake na kuichapa Benin mabao 3:0 siku ya ufunguzi jumamosi iliopita.Sdiku ya pili yake,kipa huyo anasemekana alichomwa kisu na kuuwawa.

Benin imeunda kwahivyo, Tume maalumu kuchunguza kifo chake .

Waziri wa michezo wa Kamerun, Philippe Mboa alitoa ahadi kati ya wiki hii kwa kocha mpya wa simba wa nyika, Artur Jorge kwamba serikali ya Kamerun itaacha tabia yake ya kuingilia kati katika kuchagua wachezaji wa timu ya taifa.

Jorg alichukua wiki 2 hivi nyuma wadhifa wa kuwanoa simba wsa nyika ulioachwa na kocha mjerumani Winfried Schäfer alietimuliwa Novemba mwaka jana kufuatia kushindwa kwa Simba kunguruma.

Kamerun iko pointi 4 nyuma ya Tembo wa Ivory Coast katika kinyan’ganyiro cha kanda ya Afrika kuania tikiti 5 za Kombe la dunia mwakani hapa Ujerumani.Kocha mpya amewaonya simba kwamba wanabidi kushinda mechi zao zote ikiwa wawe na tamaa ya kushiriki kwa mara ya 5 mfululizo katika Kombe la dunia la FIFA.Ikizuba mara hii itakua Tembo wa Ivory Coast watakaotia fora mwakani hapa Ujerumani.

Katika kinyan’ganyiro cha Kombe la Dunia mwaka jana huko Tunisia, rais Paul Biya aliingilia kati na kuomba mshambulizi hatari Patrick Mboma ajumuishwe na kikosi cha simba wa nyika.na nani angelithubutu kulikataa ombi la rais Biya ?

RAIS WA IOC AZURU MECCA YA RIADHA:ELDORET,KENYA:

Rais wa Halmashauri Kuu ya olimpik Ulimwenguni, Jacques Rogge akimaliza ziara yake ya siku 5 nchini Kenya, taifa kuu la riadha barani afrika, alizuru mji wa Eldoret, Mecca ya riadha nchini Kenya. Huko alikutana na vizazi 4 vya wanariadha wa Kenya ambao wamechangia mno kuisisimua m ichezo ya olimpik kuanzia 1968 pale akina Kip Keino na Benjipcho ; Amos Biwott na Ben Kogo walipotia fora katika mita 1500 na mita 3000 kuruka viunzi na hata nafutali Temu katika mita 5000.

Akifuatana na mwenyekiti wa kamati ya Taifa ya olimpik ya Kenya, Kipchoge Keino ambae wiki hii aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa ya miaka 65, Jacques Rogge aliwaambia wanariadha hao wa leo na wa zamani:

"Kuna mahala pachache duniani ambako historia ya spoti inaandikwa na mabingwa wanazaliwa:Ni Wimbledon kwa mchezo wa Tennis;Lord’s kwa mchezo wa Cricket na Olympia ,ugiriki kwa michezo ya olimpik.Eldoret,Kenya ni mojawapo ya mwahala humo mwa siri-maarufu kwa kutoa mabingwa wa riadha duniani."-alisema rais wa IOC.

Wakikutana na rais huyo wa IOC, vizazi hivyo 4 vya majogoo wa Kenya waliowika katika medani mbali m bali ulimwenguni,hawakuweza kuficha umasikini wa baadhi au wengi wao:Kwani "hakuna sifa kubwa zinazoweza kutuondolea shida zetu.Tumefanya mengi kwa nchi hii na kwa spoti ulimwenguni.Serikali yetu imetuachamkono."alinungunika mmoja wa wanariadha hao wakongwe.Akaongeza,

"Ikiwa Halmashauri Kuu ya olimpik Ulimwenguni (IOC) haiwezi kutusaidia na kutukomboa kutoka hali zetu mbaya,basi hatuna wakutuokoa."

Wengi wa wanariadha wa zamani wa Kenya waliotikisa dunia walialikwa huko Eldoret kujiunga na Kip keino na Jacques Rogge.Wengine kusiklia mdundo huo wa mgfeni maarufu ,walijitumbukiza nao.Na licha kuwa hakuwatazamia,Kip keino aliwakaribisha ukumbini.Kwahivyo, wanariadha hao,wakongwe na vijana,wakajipanga na Kip akawajulisha kwa rais wa IOC.Mkongwe wao kabisa Kiprono Maritim, mwenye umri wa miaka 76 alieshiriki katika ile timu ya kwanza ya Kenya katika michezo ya jumuiya ya madola nchini Kanada, 1954 na Olimpik huko Melbourne,Australia, miaka 2 baadae sasa mvi tele, alikuwa miongoni mwao.Hakualikwa rasmi mzee Maritim.

Kizazi cha pili ni kile cha akina Amos Biwott aliefungua mlango wa milki ya Kenya ya mbio za mita 3000 kuruka viunzi-Steeplechase pale yeye na ben Kogo katika michezo ya Olimpik ya 1968 walipomaliza wa kwanza na wapili na kuipatia Kenya dhahabu na fedha.Mwengine ni Mike Boit ambae laiti si mgomo wa Afrika huko Montreal,1976 angetawazwa pengine bingwa wa Olimpik wa mita 8oo baada ya kuipatia Kenya shaba katika michezo ya münich,1972.

Kizazi cha 3 kilichokutana huko Eldoret na rais wa IOC ni kile cha akina Moses Kiptanui alishinda mataji ya dunia ya mita 3000 kuruka viunzi 1991 na 1993 pamoja na bingwa wa olimpik wa Barcelona, 1992 Mathew Birir.Hata bingwa wa mita 10.000 wa dunia, 1991 Moses Tanui alikuwapo.

Kizazi cha 4 na cha leo kiliongozwa na mshindi pekee wa medali ya dhahabu ya olimpik kwa Kenya huko Athens, mwaka jana Ezekiel Kemboi.

Labda Keino na Dr.Mike Bopit ndio wanaoweza leo kujitapa hali zao za maisha ni bora katika mlolongo wa wanariadha hao.

Hatima ya binadamu inaamuliwa baadhi ya wakati na mahala alipozaliwa:laiti Henry Rono wa Kenya, alieweka rekodi 4 za dunia kwa muda wa siku 80,angezaliwa Ujerumani au marekani,basi angelikua leo milionea.

Tutumai kwamba IOC itazingatia hali za wanariadha hawa ambao mchango wao katika riadha-ulipo moyo na msisimko wa michezo yoyote ya olimpik ni mkubwa mno.Zama zao zilikua si za malipo kwa wanariadha-zama za amateuerism kinyume na commercialism –malipo hii leo.