1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUENOS AIRES:Cristina Fernandez De kirchner adai ushindi Argentina

29 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Bf

Cristina Fernandez De Kirchner anadai kuwa mshindi katika uchaguzi war ais nchini Argentina baada ya matokeo rasmi ya mwanzo kuonyesha amepata asilimia 42 ya kura.

Matokeo ya mwanzo ambayo hayakuwa rasmi pia yalimpa ushindi Cristina Fernandez De Kirchner ambaye ni mke war ais wa nchi hiyo Nestor Kirchner anayesifika kwa kuufufua uchumi.

Matokeo rasmi ya mwanzo yanaonyesha Cristina anaongoza dhidi ya wapinzani wake 13 katika kinyang’anyiro hicho.

Matokeo hayo yanaashiria kuwa hakutakuwepo na duru ya pili ya uchaguzi. Cristina mwenye umri wa miaka 54 huenda atakuwa mwanamke wa kwanza kuwa rais nchini humo ikiwa atatangazwa mshindi na akichukua wadhifa huo kutoka kwa mumewe.

Maafisa wa uchaguzi hapo jana iliwabidi kuongeza muda wa saa moja kwa ajili ya wapiga kura waliofika vituoni katika muda wa mwisho mwisho.