1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUENOS AIRES : Argentina yaamuru kukamatwa kwa Rais wa zamani wa Iran

10 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCuK

Hakimu nchini Argentina hapo jana ametowa hati ya kukamatwa ya kimataifa kwa Rais wa zamani wa Iran Akbar Hashemi Rafsanjani na maafisa wengine waandamizi wa serikali ya Iran kutokana na kuhusika kwao katika kuripuliwa kwa kituo cha Kiyahudi kinachoratibu shughuli za misaada nchini Argentina ambapo watu 85 waliuwawa.

Hakimu Rodolfo Canicoba Corral ameliambia shirika la habari la AFP kwamba ameiomba serikali ya Iran pamoja na polisi wa kimataifa Interpol kumkabidhi kwao rais huyo kutokana na hati ya kukamatwa kwake kwa tuhuma za kuhusika na uhalifu dhidi ya ubinaadamu katika shambulio la kituo hicho lililouwa watu 85 na kujeruhi wengine 300.

Hakuna mtu aliyewahi kupatikana na hatia ya kuripua kituo hicho hapo mwezi wa Julai mwaka 1994.