1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUDAPEST: Waziri mkuu wa Hungary agoma kujiuzulu

20 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDAp

Polisi nchini Hungary wamewatawanya waandamanaji hii leo na kutuliza ghasia zaidi zilizozuka katika mji mkuu wa Hungary Budapest baada ya polisi kupambana na waandamanaji hao usiku mzima.

Waziri mkuu wa nchi hiyo Ferenc Gyurcsany amesema hatojiuzulu na ataendelea na mageuzi makali ya kiuchumi licha ya kufanyika maandamano ya kumtaka ajiuzulu hapo jumatatu.

Watu kati ya 2000 hadi 3000 wakiwemo wazalendo wa mrengo wa kati-kulia walivamia jengo la televiesheni ya taifa na kumtaka waziri mkuu huyo ajiuzulu.

Ghasia hizo zilizuka kufuatia kufichuka kwa taarifa zilizorekodiwa kwenye mkanda wa sauti ambapo waziri mkuu Ferenc alikiri chama chake kilisema uongo juu ya uchumi wa nchi ili kujipatia ushindi katika uchaguzi wa mwezi Aprili.