1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Budapest: Mafuriko makubwa katika Hungary

18 Aprili 2006
https://p.dw.com/p/CBJ1

Wakuu huko Hungary wanasema mto wa pili kwa ukubwa katika nchi hiyo, Tisza, umefikia kima cha juu kabisa na mafuriko ya mto huo sasa yanawahatarisha watu 160,000 waliko katika nyumba 50,000. Wiki mbili zilizopita, Mto Danube ulifikia kiwango cha juu kabisa cha Mita 8.6 huko Budapest. Maji ya mto huo yamepungua sasa huko Hungary, lakini yamesababisha mafuriko makubwa huko Serbia na Romania. Maelfu kwa maelfu ya watu wameshahamishwa kutoka maeneo yao na hali ya hatari imetangazwa katika maeneo yalio karibu na Mto Danube. Mabingwa wanasema vima vya maji vinatarajiwa kufikia kilele hapo kesho.